1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spian ni timu bora ya dunia

2 Julai 2008

Orodha mpya ya FIFA imeiweka Spain,mabingwa wa Ulaya kileleni.

https://p.dw.com/p/EUxC

Spain iliotawazwa jumapili mabingwa wa kombe la Ulaya la dimba, sasa imeparamia kileleni mwa ngazi ya FIFA kuwa ndio timu bora kabisa duniani.Hii ikiwa ni mara ya kwanza katika historia yake.Stadi wa FC Barcelona, mkamerun Samuel Eto'o, atashiriki katika mashindano ya timu 4 kufungua pazia la dimba la olimpik huko Hong kong,China.Na bingwa wa rekodi ya dunia ya mita 100 Usain Bolt pamoja na bingwa wa zamani Asafa Powell, ni miongoni mwa majina makubwa ya wanariadha watakoiwakilisha Jamaica huko Beijing kuania medali za Olimpik .

Mzee Luis Aragones -kocha wa Spian alieitawaza timu yake majuzi mabingwa wa Ulaya baada ya kuikomea Ujerumani bao 1:0, yaonesha hajakosea alipodai Spian sasa sio tu mabingwa wa Ulaya,bali ni timu bora ya dunia.

Orodha ya FIFA -shirikisho la dimba ulimwenguni iliotoka hivi hivi punde imeipandisha Spian kileleni kwa mara ya kwanza katika historia yake ya dimba.Spian kwahivyo, imeipokonya Itali, mabingwa wa dunia usukani .Ujerumani,ilioibuka makamo-bingwa wa Ulaya nyuma ya Spain, imeangukia nafasi ya 3.

Brazil iko nafasi 4 wakati Holland,timu nyengine mbali na Spain ilizikosha nyoyo za mashabiki wa dimba wa Ulaya iko nafasi ya 5.Makamo-bingwa wa dunia,Ufaransa imetupwa sasa safu ya 10 ikija baada ya Ureno.

Kocha wa Spain, mzee Luis Aragones atakaekuwa sasa kocha wa klabu ya Fernabahce ya Uturuki,amefichua kuwa ameaamua kutoendelea kuwa kocha wa Spian kwa kuwa shiorikisho la dimba la nchi hiyo RFEF halikutaka yeye abakie.

Mzee Aragones, akiwa na umri wa miaka 69, aliongoza Spain kukata kiu cha miaka 44 cha kutawazwa mabingwa wa Ulaya.Fernabahce ya Uturuki, ilikwishafunga mkataba wa miaka 2 hata kabla kumalizika kombe la ulaya.

Vyombo vya habari vya Spian vimearifu kwamba, kocha wa zamani wa Real Madrid,Vicente del Bosque ndie atakaeshika sasa hatamu zilizoachwa na mzee Aragones.

Mkamerun,anaeichezea FC Barcelona ya spain, Samuel Eto'o atashiriki katika mashindano ya dimba ya timu 4 kufungua pazia la michezo ijayo ya olimpik huko Hong Kong, china.Eto'o ameteuliwa na simba wa nyika kuania kombe la ING cup litakalojumuisha pia Holland,Marekani na Ivory Coast.Timu zote hizo 4 zitaania medali ya dhahabu hapo August katika dimba la olimpik mjini Beijing.Kila timu ya wachezaji 18 ya olimpik ina nafasi ya kuwachagua wachezaji 3 maarufu huku walioasalia wasizidi umri wa miaka 23.

Eto'o bado hajui ataichezea klabu gani msimu ujao baada ya Barcelona kusema itayari kumuachia aondoke.

FC Cologne, iliopanda tena msimu ujao daraja ya kwanza ya Bundesliga,inapigania kumrejesha stadi wake wa zamani aliejiunga na Bayern Munich-Lukas Podolski. Kocha wa FC Cologne, Christoph Daum ameliambia gazeti la express kuwa endapo Bayern munich, itatoa ishara kuwa Podolski anaweza kuwaacha mkono, basi cologne itayari kumuajiri tena.Moyo wa podolski upo Cologne,maskani yake.Alijiunga na munich baada ya cologne, kuteremshwa daraja ya pili mwaka juzi.

Riadha:

Jamaica,mojawapo ya mataifa makuu ya riadha ulimwenguni na hasa masafa mafupi tangu upande wa wanawake na hata wa wanaume, imetangaza baadhi ya majogoo wake inaotumai watawika katika michezo ijayo ya olimpik ya Beijing:

Wanajumuisha upande wa wanaume, bingwa wa sasa wa rekodi ya duniaya mita 100 Usain Bolt,bingwa wa zamani wa rekodi hiyo Asafa Powell na bingwa wa sasa wa olimpik wa masafa ya mita 200 wanawake Veronica Campbell-Brown.

Bolt aliekimbia muda wa sek.9.72 hapo Mei 31 mjini New York na kuivunja rekodi ya Asafa Powell ya sek.9.74 pamoja na Campbell ndio wanaotazamiwa sana kurudisha Jamaica medali za dhahabu,fedha na shaba.

►◄