1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirikisho la DFB lachunguzwa kwa udanganyifu wa kodi

7 Oktoba 2020

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamefanya upekuzi katika makao makuu ya ofisi za Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) pamoja na nyumba za wajumbe wa chama hicho kufuatia uchunguzi wa udanganyifu wa kukwepa kulipa kodi.

https://p.dw.com/p/3jZzD
Deutschland Frankfurt Durchsuchung beim DFB
Picha: Frank Rumpenhorst/dpa/picture-alliance

Waendesha mashtaka mjini Frankfurt wamesema makao makuu ya Chama cha Soka cha Ujerumani (DFB) ambalo ni moja kati ya mashirikisho makubwa ya michezo ulimwenguni pamoja na nyumba za maafisa wa DFB zimepekuliwa  kwa tuhuma za kukwepa kodi.

Msako huo ulifanywa katika majimbo matano kote Ujerumani ambayo ni Hesse, Bavaria, North-Rhine Westphalia, Lower Saxony na Rhineland-Palatinate.

Takriban maafisa 200 walishiriki katika zoezi hilo na miongoni mwao wakiwa maafisa wa kukusanya ushuru na maafisa wa polisi.

Uchunguzi umeelekezwa kwa kiasi kikubwa dhidi ya maafisa watendaji sita wa zamani au wa sasa wa DFB. Wanashutumiwa kwa kutangaza kimakosa kwa makusudi mapato ya matangazo katika 2014 na 2015 kwenye michezo ya nyumbani ya timu ya kitaifa. Mashtaka hayo yanahusiana na matangazo ya mzunguko katika viwanja vya michezo.

Deutschland Frankfurt Durchsuchung beim DFB
Maafisa wa polisi wakiwa wamesimama nje ya ofisi za makao makuu ya DFB, kufuatia tangazo kwamba polisi imevamia ofisi na makaazi wa wanchama wa juu, kuhusiana na uwezekano ukwepaji mkubwa wa kodi, Oktoba, 07, 2020.Picha: Thomas Lohnes/Getty Images

Inaarifiwa kuwa kiasi cha ushuru kilichokwepwa kinaweza kuzidi euro milioni 4.7

Soma zaidi: Mgombea wa urais Groth aukosoa uongozi wa DFB

Katika taafira kutoka katika shirikisho hilo uchunguzi unaashiria kuwa watuhumiwa hao walifahamu kuwa kulikuwa na shakashaka katika marejesho lakini hawakuchukua hatua kwa lengo la kuipatia DFB faida kubwa ya ushuru.

Hata hivyo watu hao sita hawakutajwa.

Hii ndio kesi ya hivi karibuni katika mfululizo wa kesi za kisheria ambazo chama kikubwa cha mpira wa miguu kimepatikana katika siku za hivi karibuni. Awali uchunguzisawia na huo ulifanywa wakati wa Kombe la Dunia la 2006 kwa Ujerumani na jinsi pesa zilivyotumiwa katika kuelekea mashindano hayo.

Hivi karibuni DFB  ilifikisha mwisho ushirikiano wake na wakala wake wa uuzaji baada ushirikiano wa takriban miaka 40 baada ya ripoti kuibuka kwa makosa ya kifedha.

Chanzo: DW