Serikali ya Somalia yavunjwa wiki mbili baada ya kuundwa | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Serikali ya Somalia yavunjwa wiki mbili baada ya kuundwa

Baidoa:

Waziri mkuu Nur Hussan Husssein wa Somalia amelivunja baraza lake la mawaziri hii leo,wiki mbili baada ya mwaziri wake watano kujiuzulu.Katika mkutano na waandishi habari mjini Baidoa,waziri mkuu Hussan Hussein amesema serikali mpya itateuliwa wiki mbili kutoka sasa.”Nimeamua kuunda serikali ambayo asili mia 50 ya mawaziri watakua wabunge”-amesema waziri mkuu huyo.Tangu alipoteuliwa mwezi uliopita,Hussein amekua akizongwa na mivutano ya ndani katika serikali ambayo bado haijapata ridhaa ya bunge,tangu ilipoundwa december pili iliyopita.Wakati huo huo Mouktar Ali Ropbow,kiongozi mmojawapo wa waasi wa kiislam,anaeishi mafichoni amesema chama chake cha Al Chabab kitazidisha harakati dhidi ya vikosi vya serikali na washirika wao wa Ethiopia..Watu elfu sita wameuwawa nchini Somalia mwaka huu,kufuatia mapigano na mashamnbulio ya kuyatolea mhanga maisha.

 • Tarehe 16.12.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcLA
 • Tarehe 16.12.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcLA

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com