Serikali ya China yashutumu maandamano. | NRS-Import | DW | 25.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Serikali ya China yashutumu maandamano.

Beijing.

Serikali ya China imeshutumu maandamano dhidi ya China wakati wa sherehe za uwashaji wa mwenge wa Olimpiki na kusema kuwa ni kitendo cha aibu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Beijing ameyataka mataifa duniani ambayo mwenge wa Olimpiki utapitia kuhakikisha kuwa unapita kwa salama.

Jana Jumatatu , wanaharakati wanaounga mkono Tibet walijaribu kuharibu sherehe hiyo nchini Ugiriki ya kuwasha mwenge wa Olimpiki.

Hali ya wasi wasi wakati huo huo imeendelea ndani na nje ya jimbo la Tibet.

Kuna ripoti za hali zaidi ya ghasia na watu 13 wamekamatwa katika mji mkuu wa Tibet wa Lhasa.

Serikali ya Tibet iliyoko uhamishoni inasema kuwa imeweza kuthibitisha kuwa watu 140 wameuwawa katika ghasia hizo, zilizoanza March 10.

Serikali ya China imeripoti watu 19 kuwa wameuwawa, lakini idadi hizo zote hazikuweza kuthibitishwa na duru huru. Nchini Nepal , polisi wamewakamata zaidi ya Watibet 100 ambao waliandamana mbele ya ofisi ya kutolea visa ya ubalozi wa China katika mji mkuu Kathmandu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com