Serikali mpya ya Palastina yaanza shughuli zake | Habari za Ulimwengu | DW | 18.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Serikali mpya ya Palastina yaanza shughuli zake

Gaza:

Serikali mpya ya Palastina inaanza shughuli zake hii leo baada ya kuidhinishwa na bunge jana.Umoja wa Ulaya umeikaribisha serikali hiyo ya Umoja wa taifa iliyoundwa na Hamas na Fatah.Ujerumani ,mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya imesema katika taarifa mjini Berlin,itahitaji kuona vitendo vya serikali mpya kabla ya kuamuliwa kama misaada ya fedha iendelee kutolewa au la.Marekani nayo pia imeelezea shaka shaka zake.Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Sean McCormack ameitaja hoja ya waziri mkuu Isamael Hanniya” juu ya “haki ya kuendeleza mapambano kua ni yenye kuvunja moyo.”Israel nayo pia imesema haitaitambua serikali mpya ya Palastina.Norway inataka kuitambua serikali hiyo nazo Urusi na Ufaransa zimelezea utayarifu wa kushirikiana na serikali hiyo mpya ya Palastina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com