Serikali Mpya ya Italia | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.11.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Serikali Mpya ya Italia

Mario Monti apewa jukumu la kuunda serikali mpya

default

Waziri Mkuu mpya wa Italia Mario Monti

Waziri Mkuu wa mpya wa Italia Mario Monti amepewa jukumu la kuunda serikali baada ya Silvio Berlusconi kujiuzulu.

Rais wa Italia Giorgio Napolitano amearifu hayo baada ya kukutana kwa siku nzima hapo jana na wawakilishi muhimu wa vyama na wabunge.

Serikali mpya itakayoongozwa na Waziri Mkuu Mario Monti, mtu mwenye hadhi kubwa duniani ya utaalamu wa masuala ya uchumi itakuwa na jukumu la kuirejesha imani ya wawekaji vitega uchumi kwenye masoko ya fedha na kuindoa Italia kutoka kwenye mgogoro wa madeni.

Hapo jana baada baraza la Seneti, bunge pia liliupitisha mpango wa kubana matumizi ambao Italia inatakiwa iutekeleze na Umoja wa Ulaya.

.

 • Tarehe 14.11.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/13A3b
 • Tarehe 14.11.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/13A3b

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com