1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serbia kuchukua hatua ya kisheria kuhusu Kosovo

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZyY

Serbia itakwenda mbele ya Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague,Uholanzi iwapo jimbo la Kosovo lililojitenga litatangaza uhuru wake.Rais Boris Tadic alitamka hayo kwenye televisheni ya Serbia na kuongezea kuwa Mahakama ya Kimataifa itapaswa kuamua ikiwa hatua hiyo ni halali.

Kwa upande mwingine,msemaji wa viongozi wa Kosovo wenye asili ya Kialbania aliwaambia waandishi wa habari mjini Pristina kuwa watajitangazia uhuru wao,ifikapo mwezi wa Aprili.Marekani na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zimesema,zitatambua Kosovo iliyo huru.Lakini Urusi kama mshirika wa Serbia imesema haitoiruhusu Kosovo kutangaza uhuru wake bila ya idhini ya Serbia.