1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Silaha za Ujerumani zisitumike kufanya mashambulizi Urusi

27 Mei 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kwamba silaha zinazotolewa na nchi yake kwa Ukraine hazipaswi kutumika katika mashambulizi kwenye ardhi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4Rt41
Estland | Bundeskanzler Scholz in Tallinn
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Scholz ameyasema hayo siku ya Ijumaa akiwa ziarani katika mji mkuu wa Estonia Tallin na kuongeza kwamba silaha wanazozitoa ni kwa ajili ya Ukraine kujilinda pekee.

Mwanzoni mwa mwaka, Scholz alisema kulikuwa na "makubaliano" na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwamba,silaha za Ujerumani hazitatumika kwa mashambulio kwenye eneo la Urusi.

Soma zaidi: Scholz atangaza nchi yake itapeleka silaha zaidi UkraineKauli ya Kansela Scholz mara kadhaa imerudiwa na Marekani ikiwemo mnamo siku ya Alhamisi ambapo msemaji wa Ikulu ya White House John Kirby alisema vifaa vilivyotengenezwa na Marekani, vinavyotolewa na Marekani havitakiwi kutumika katika kuishambulia Urusi.