1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAULO: Maandamano ya kuipinga ziara ya Bush yafanyika

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKm

Waandamanaji wamekusanyika nje ya kiwanda cha kusambaza mafuta kupinga ziara ya rais wa Marekani, George W Bush, nchini Brazil hii leo. Brazil ni kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya mataifa matano ya Amerika Kusini.

Waandamanaji walibeba mabofu yaliyokuwa na maandishi kwa lugha ya kiingereza na kireno ya kumtaka rais Bush aondoke nchini humo kwa matumaini kiongozi huyo angeyaona wakati wa mkutano wake na rais wa Brazil, Ignacio Lula da Silva, katika kiwanda hicho.

Viongozi hao walitarajiwa kusaini mkataba wa matumizi ya mafuta aina ya ethanol.

Hapo awali watu zaidi ya 20 walijeruhiwa kwenye maandamano yaliyoshuhudia mapigano baina ya polisi na waandamanji mjini Sao Paulo.

Ziara ya rais Bush inafanyika wakati rais wa Ujerumani, Hosrt Köhler, akiendelea za ziara yake nchini Brazil.

Nchini Colombia ambako rais Bush anatarajiwa kuwasili keshokutwa Jumapili, wanafunzi, wafuasi wa vyama vya upinzani na wanachama wa vyama vya wafanyakazi wamekuwa wakifanya maandamano kwa siku mbili kuipinga ziara ya Bush nchini humo.