Sakaya:Chama cha CUF hakijatoka UKAWA | Matukio ya Afrika | DW | 15.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Sakaya:Chama cha CUF hakijatoka UKAWA

Chama cha wananchi CUF nchini Tanzania ambacho ni miongoni mwa vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kimekanusha kususia vikao vya umoja huo kikisema kwanza kinataka kurejea katika katiba yake.

Magdalena Sakaya Pressekonferenz Civic United Front

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha CUF upande wa bara, Magdalena Sakaya, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam (15.07.2015)

Chama hicho kinatakakurejea katika katiba yake ili kiweze kufanya maamuzi kwa mujibu wa msingi wa katiba yake. Haya yanajiri baada ya baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuripoti kuwa chama hicho kimejiengua kutoka katika umoja huo kwa madai kuwa chama hicho hakijapewa nafasi ya kuteuwa mgombea ikizingatiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho profesa Ibrahim Lipumba ana sifa za kuwakilisha umoja huo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Hawa Bihoga kutoka Dar es salaam kwa kubonyeza alama za spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Hawa Bihoga
Mhariri:Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com