1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Edward Lowassa

Edward Ngoyai Lowassa ni mwanasiasa wa Tanazania aliekuwa waziri mkuu wa Jamhuri kati ya mwaka 2005 na 2008, akihudumu chini ya rais Jakaya Kiwete.

Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953, na ameweka rekodi ya kuwa waziri mkuu wa kwanza kulazimishwa kujiuzulu kutokana na sakata la rushwa katika historia ya Tanzania. Kufuatia kujiuzlu kwake, rais Kikwete alitakiwa kulivunja baraza la mawaziri, na kuunda jipya chini ya waziri mkuu mpya Mizengo Pinda. Baada ya CCM kukataa kumteuwa kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Lowassa alikihama chama hicho na kujiunga na chama kikuu cha upinzani Chadema, alikogombea. Alishindwa na mgombea wa CCM John Magufuli.