Edward Lowassa arejea CCM | Matukio ya Afrika | DW | 01.03.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Edward Lowassa arejea CCM

Mwanasiasa wa Upinzani nchini Tanzania Edward Lowasa ametangaza kujiunga tena na chama tawala nchini humo CCM kiasi miaka minne tangu alipohamia upinzani na kuwania kiti cha urais mwaka 2015.

Rais John Magufuli wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala nchini humo amemkaribisha bw Lowasa kurejea CCM katika tukio la wazi lililofanyika hivi leo kwenye ofisi ndogo za chama cha mapinduzi mjini Dar es Salaam.

Katika maelezo mafupi aliyoyatoa mbele ya wafuasi wachache wa Chama cha Mapinduzi walioshuhudia kurejea kwake kwenye chama hicho, Lowasa amesema  ´´Nimerejea nyumbani``

Lowasa alijiunga na upinzani mwaka 2015 siku chache baada ya kukosa nafasi ya kuwania kiti cha urais ndani ya Chama cha Mapinduzi

Akizungumza na DW muda mchache baada ya taarifa za Lowasa kurejea CCM, Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema  Vincent Mashinji amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa mshtuko lakini akaonegza kuwa hamlaumu Lowasa kwa kuwa huo ni uamuzi binfasi na ni sehemu ya haki zake.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hatua ya wanasiasa wa upinzani kuhamia ndani ya chama tawala inadidimiza demokrasia katika taifa hilo la Afrika Mashariki.