1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Tundu Lissu

Tundu Antiphas Mughwai Lissu, ni mwanasheria wa Tanzania, mwanasiasa wa CHADEMA na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki tangu 2010. Ni Rais wa chama cha Wanasheria cha Tanzania (TLS) na mwanasheria mkuu wa CHADEMA.

Kwa miaka kadhaa sasa, Lissu amejijengea sifa kama wakili mashuhuri, mwanasiasa shupavu wa upinzani na mkosoaji mkuu wa serikali, na kutokana na makabiliano yake na serikali ya Rais John Magufuli. Lissu alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma na kujeruhiwa vibaya Septemba 7, 2017, na watu wasiojulikana. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu Tundu Lissu.

Onesha makala zaidi