1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

CHADEMA

Chadema ndiyo chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Ni chama kinachofuata nadharia za mrengo wa wastani wa kulia. Jina lake ni kifupi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Chadema iliasisiwa mwaka 1995 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania. Waasisi wake ni mzee Edwin Mtei, gavana wa zamani wa benki kuu ya Tanzania na Mzee Bob Makani. Ni chama kinachowavutia zaidi vijana na wasomi nchini Tanzania na kimekuwa kikiongezeka umaarufu kadiri siku zinavyokwenda na kuwa nguvu ya pili kwa chama tawala CCM. Katika ukurasa huu utapata maudhui za DW zinazohusiana na Chadema.

Onesha makala zaidi