Rwanda yapiga marufuku adhabu ya kifo | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Rwanda yapiga marufuku adhabu ya kifo

Uamuzi wa Rwanda kuondosha adhabu ya kifo umekaribishwa na Umoja wa Mataifa na shirika linalogombea haki za binadamu duniani-Amnesty International.

Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Bibi Louise Arbour

Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Bibi Louise Arbour

Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Bibi Louise Arbour amesema,hatua hiyo inafungua njia ya kuwafikisha mahakamani washukiwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda,ambako kiasi ya watu 800,000 waliuawa katika mwaka 1994.

Shirika la Amnesty International limesema,Rwanda imekuwa nchi ya kwanza katika kanda ya Maziwa Makuu,kupiga marufuku adhabu ya kifo na kuthibitisha mwenendo wa dunia nzima,kukomesha adhabu ya kifo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com