1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda na nchi nyingine 11 kupata dozi za Lenacapavir

15 Aprili 2026

Rwanda na mataifa mengine 11 duniani yatanufaika na ufadhili mpya wa Marekani utakaosaidia upatikanaji wa dawa ya sindano za kuzuia maambukii ya virusi vya UKIMWI iliyoidhinishwa hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/5CB0m
Dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU, Lenacapavir
Dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU, Lenacapavir. Picha: Nardus Engelbrecht/AP Photo/picture alliance

Kupitia ushirikiano wa Marekani na shirika la Global Fund zaidi ya watu wengine milioni moja duniani watapatiwa dawa hiyo iitwayo Lenacapavir.

Hapo kabla Marekani ilifadhili utoaji dawa hiyo kwa watu milioni mbili katika mataifa 9 duniani. Ufadhili mpya uliotangazwa jana, umeziongeza nchi nyingine 12 ikiwemo Rwanda, Morocco, Thailand, Fiji na Jamhuri ya Dominica.

Wanasayansi wanasema dawa hiyo inayotolewa mara mbili kwa mwaka kwa njia ya sindano imethibitika kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia 99.9.