1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuipima Urusi kama ina nia ya kumaliza vita Ukraine

14 Februari 2026

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio amesema hii leo kwamba nchi yake itaendelea kushinikiza upatikanani wa makubaliano ya amani ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/58l5G
Deutschland München 2026 | US-Außenminister Marco Rubio bei der Münchner Sicherheitskonferenz
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco RubioPicha: dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Marekani imesema inabidi ipime na kuangalia kwanza iwapo kweli Urusi inataka kusitisha vita vyake huko.

Akizungumza katika mkutano wa usalama unaofanyika Munich Ujerumani, Rubio amesema hawana hakika iwapo Urusi ina nia ya kweli ya kusitisha vita hivyo, lakini Marekani itaendelea kuishinikiza ili kukomesha vita hivyo vitakavyoingia mwaka wake wa tano hivi karibuni.

Huku hayo yakiarifiwa nchini Ukraine kwenyewe shambulizi la Urusi lililotokea usiku wa kuamkia leo mjini Odesa lililenga jesngo la wakaazi na kusababisha kifo cha mwanamke mmoja, hii ikiwa ni kulingana na gavana wa eneo hilo la Kusini mwa Ukraine.