Ruanda: Wafungwa wagoma kutokana na huduma mbaya ya Chakula
28 Septemba 2009Matangazo
Katika gereza la Rusizi
kusini mwa nchi hiyo wafungwa walisema matatizo ya chakula
yamekuwepo kwa muda wa mwezi mzima. Viongozi wa magereza
nchini humo wamekiri kutokea matatizo ya chakula, lakini
wakasisitiza kuwa machafuko yalichochewa na wafungwa wenye
vurugu. Kwa sasa hali imetulia baada ya mazungumzo baina ya pande
zinazohusika.
Mwandishi wetu kutoka Kigali, Rwanda, Daniel Gakuba ana maelezo zaidi:
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mtayarishaji: Grace Patricia Kabogo
Mhariri: Thelma Mwadzaya