Rome. Wateka nyara watakiwa kuhakikisha kuwa mateka wao yu hai kabla ya majadiliano. | Habari za Ulimwengu | DW | 11.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rome. Wateka nyara watakiwa kuhakikisha kuwa mateka wao yu hai kabla ya majadiliano.

Italia inasema kuwa wapiganaji ambao wamemteka nyara mwandishi habari raia wa Italia nchini Afghanistan wanapaswa kuhakikisha kuwa bado yu hai kabla ya kuanza kwa majadiliano yoyote juu ya kuachiwa kwake.

Waasi wa taliban wanadai kuwa wamemkamata Daniele Mastrogiacomo, mwandishi anayefanyakazi na gazeti la kila siku la La Republica, pamoja na Waafghani wawili ambao walikuwa wanasafiri nae katika wilaya ya Nadi Ali katika jimbo la Helmand siku ya Jumatatu.

Balozi wa Italia mjini Kabul amesema kuwa anamatumaini kuwa wateka nyara hao wako tayari kuanza majadiliano ambayo yatafanyika chini ya msingi kwamba itathibitishwa kuwa mwandishi huyo yuko hai.

Wakati huo huo, taarifa ya wizara ya wizara ya mambo ya kigeni ya Italia imethibitisha kuwa Mastrogiacomo yu hai.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com