RIYADH:Mataifa ya kiarabu yatia juhudi kufikia muafaka | Habari za Ulimwengu | DW | 28.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH:Mataifa ya kiarabu yatia juhudi kufikia muafaka

Viongozi wa mataifa ya Arabuni wanaanza mkutano unaolenga kufufua mazungumzo ya kutafuta amani ya Mashariki ya kati mjini Saudia hii leo. Mkutano huo unafanyika kukiwa na hali ya wasiwasi katika eneo hilo baada ya nchi ya Iran kukataa kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium kama ilivyoagizwa na Umoja wa mataifa.Viongozi wa eneo hilo wana hofu kuwa hilo huenda likasababisha kushambuliwa na Marekani jambo ambalo huenda likasababisha vurugu zaidi.

Kikao hicho cha siku mbili kinahudhuriwa na wafalme wa mataifa ya kiarabu vilevile marais kinalenga kurejesha uhusiano mzuri na taifa la Israel endapo litakubali kujiondoa katika eneo la palestina vilevile kukubali kuundwa kwa taifa la Palestina.

Mfalme Abdulla wa Jordan alifanya mikutano na viongozi wa mataifa ya Kiarabu jana usiku akiwemo Bashar al Assad wa Syria ambao mpaka sasa uhusiano wao si mzuri kwasababu ya nchi yake kuunga mkono kundi la Hezbollah la Lebanon vilevile nchi ya Iran.

Mpango wa kutafuta amani ya mashariki ya kati wa mataifa ya kiArabu unakubalika na wote….kwa sasa jamii ya kimataifa inautambua na hata waIsraeli wenyewe wanaona manufaa yake.Nadhani kama washiriki wakuu wana nia ya kupata amani mpango huu huu utafanikisha lengo hilo kwa wote vilevile kuleta ustawi katika eneo la Mashariki ya kati.

Mkutano huo aidha unalenga kutoa wito wa kuondolewa vikwazo vya fedha na kidiplomasia ilivyowekewa Palestina tangu chama cha Hamas kuingia madarakani mwaka mmoja uliopita.Kwa upande mwingine kikao hicho kinataraji kufikia azimio litakalosababisha mabadiliko kufanywa katika katiba ya Iraq ili kuwapa madaraka zaidi Wasunni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com