RIYADH:Kansela Merkel aendelea na ziara ya mashariki ya kati nchini Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 05.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH:Kansela Merkel aendelea na ziara ya mashariki ya kati nchini Saudi Arabia

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani yupo nchini Saudi Arabia kuendelea na ziara ya siku nne katika mashariki ya kati.Kansela Merkel anafanya ziara hiyo kwa lengo kuzitia msukumo mpya juhudi za kuanzisha tena mazungumzo ya kuleta amani baina ya wapalestina na waisraeli.

Bibi Merkel amewasili Saudi Arabia kutokea Misri ambapo alifanya mazungumzo na katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu bwana AMR MOUSSA na rais Hosni Mubarak.

Kiongozi huyo wa Ujerumani pia atazitembelea Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com