RIYADH: Steinmeier akamilisha ziara ya Mashariki ya Kati | Habari za Ulimwengu | DW | 09.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH: Steinmeier akamilisha ziara ya Mashariki ya Kati

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekamilisha ziara yake ya Mashariki ya Kati kwa kukutana na Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba(AGCC) mjini Riyadh, Saudi Arabia.Majadiliano hayo yaliohusika na biashara kati ya nchi za Umoja wa Ulaya na nchi za Ghuba,yaligubikwa na khofu kuhusika na mpango wa amani wa Mashariki ya Kati.Waziri wa kigeni wa Saudi Arabia,Mwana-mfalme Saud al-Faisal amesema, majadiliano hayo ya amani yapo katika hali iliyo mbaya sana.Wakati huo huo waziri Steinmeier amesema,anaunga mkono juhudi za amani zinazoongozwa na nchi za Kiarabu,zikitoa uwezekano wa kuitambua rasmi Israel pindi nchi hiyo itaondoka kutoka maeneo iliyoyavamia mwaka 1967 na pia kukubali haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea makwao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com