RIYADH: Migogoro ya kidini isiruhusiwe kusambaa
4 Machi 2007Matangazo
Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran na Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia wamekubali kushirikiana kuzuia mgogoro unaohusika na madhehebu ya Kiislamu nchini Irak,kuenea katika maeneo mengine ya kanda hiyo.Kwa mujibu wa shirika la habari la Saudi Arabia,viongozi hao wawili walipokutana mjini Riyadh,walisisitiza pia umuhimu wa kuwepo umoja wa Wapalestina na haja ya kuhifadhi uhuru na umoja wa Irak.