1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIO DE JANEIRO: Ajali ya treni yasababisha vifo

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUK

Watu wasiopungua 8 wameuawa na kiasi ya 70 wengine wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea nje ya mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil.Kwa mujibu wa msemaji wa Super via,treni ya shirika hilo iliyokuwa na kama abiria 850 iligongana na treni nyingine iliyoegezwa na ambayo haikuwa na abiria.Kuna hofu kuwa idadi ya wahanga huenda ikaongezeka kwa sababu abiria wengi wamenasa ndani ya mabehewa.