Riadh. Watuhumiwa kadha wakamatwa kabla ya kufanya shambulio. | Habari za Ulimwengu | DW | 03.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Riadh. Watuhumiwa kadha wakamatwa kabla ya kufanya shambulio.

Maafisa nchini saudi Arabia wamesema kuwa wamezuwia shambulio, baada ya kuwakamata zaidi ya watuhumiwa 130 katika muda wa miezi mitatu iliyopita.

Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa watuhumiwa, wengi wao wakiwa ni raia wa Saudia , wanahusiana na vikundi ambavyo vina maingiliano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda. Wameongeza kuwa kikundi kimoja kilikuwa kinapanga shambulizi hivi karibuni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com