Riadh. Pelosi analiza ziara yake ya mashariki ya kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Riadh. Pelosi analiza ziara yake ya mashariki ya kati.

Spika wa baraza la wawakilishi nchini Marekani , Nancy Pelosi kutoka chama cha Democratic , amekutana na baraza la kisiasa la ushauri nchini Saudi Arabia wakati wa ziara yake ya mashariki ya kati.

Pelosi alitembelea baraza hilo la ushauri wa kisiasa ambalo huteuliwa na mfalme Abdullah wa Saudi Arabia .

Pelosi amewasili nchini humo akitokea Syria, ambako amekaidi sera za Ikulu ya Marekani kuelekea mashariki ya kati kwa kukutana na rais wa Syria Bashar al-Assad.

Pelosi amesema Assad amemwambia kuwa Syria iko tayari kuanza tena majadiliano ya amani na Israel. Serikali ya rais wa Marekani imemshutumu Pelosi kwa kufifisha juhudi za kuutenga utawala wa rais Assad kwa madai ya kuunga mkono ugaidi pamoja na kile kinachosemekana kuwa ni kuingilia mambo ya ndani ya Iraq na Lebanon.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com