Ramallah. Steinmeier ziarani mashariki ya kati.
5 Mei 2007Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amewasili katika mamlaka ya Palestina kama sehemu ya ziara yake katika mashariki ya kati.
Mjini Bethlehem alizungumza na wawakilishi wa jumuiya ya kibiashara ya Palestina. Leo Jumamosi Steinmeier atakuwa na mazungumzo na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.