RAMALLAH: Silaha bila ya vibali zapigwa marufuku
27 Juni 2007Matangazo
Rais Mahmoud Abbas,amepiga marufuku kwa wapalestina kubeba silaha au miripuko bila ya kuwa na vibali.Hii ni miongoni mwa hatua mpya zenye azma ya kupunguza nguvu za makundi ya wanamgambo wa Hamas,katika Ukingo wa Magharibi. Rais Abbas ametangaza idadi kadhaa ya amri,tangu kuvunja serikali iliyokuwa ikiongozwa na Hamas, baada ya kundi hilo kwa nguvu kulitia mikononi eneo la Ukanda wa Gaza.