1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier yuko Jordan kwa mazungumzo na mfalme Abdulla II

18 Februari 2026

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amemaliza ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati leo Jumatano kwa kuitembelea Jordan anakotarajiwa kuwa na mazungumzo na mfalme Abdulla wa II.

https://p.dw.com/p/58yMg
Deutschland Berlin 2025 | Steinmeier warnt am 9. November vor Gefahren für die Demokratie
Rais wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Maryam Majd/AP Photo/dpa/picture alliance

Mazungumzo ya viongozi hao wawili yanatarajiwa kutuwama katika mzozo wa Mashariki ya kati na mpango wa usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Katika mazungumzo hayo, rais Steinmeier pia anapanga kupongeza juhudiza serikali ya Jordan za kuridhia kuwapokea wakimbizi wa Syria na wale wa kipalestina.

Rais huyo wa Ujerumani anatarajiwa pia kuzuru kituo cha usajili cha wakimbizi kinachosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR. Kulingana na shirika hilo, Jordan ni moja ya nchi iliyo na idadi kubwa ya wakimbizi duniani.

Hii leo Jioni Steinmeier na mkewe Elke Büdenbender watarejea nyumbani Ujerumani,  baada ya ziara yao ya siku tatu Mashariki ya kati.