1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia Suluhu akutana na vyama vya siasa

Kisuaheli3 Januari 2023

Rais wa Tanzanian Samia Suluhu Hassan leo, anaongoza majadiliano na wakuu wa vyama vya siasa katika mkutano unaofanyika katika ikulu mjini Dar es Salaam.

https://p.dw.com/p/4Lfzs
Belgien, Brüssel | Samia Suluhu Hassan, Präsidentin von Tansania in Brüssel
Picha: Sudi Mnette/Mohammed Khelef/DW

Mkutano huo ni mwendelezo wa majadiliano ya ngazi ya juu yaliyoanzishwa na rais Samia tangu alipoingia madarakani mwaka 2021, umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ikiwemo chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA ambacho mara zote kimekuwa kikikosoa mienendo ya serikali hasa linapokuja suala la democrasia.

 Miongoni mwa hoja ambazo zinatarajiwa kuchukua muelekeo mpya baada ya majadiliano hayo , ni pamoja na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, marekebisho ya katiba pamoja na sheria kandamizi ambazo zinaongoza shughuli za vyama vya siasa.

Kwa takriban miaka mitano, vyama vya upinzanni nchini humo vimekuwa vikilalamika kukandamizwa na dola, hatua inayotajwa kuzorotesha ushiriki kamili wa shughuli za kidemocrasia katika taifa hilo la Afrika mashariki.