1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais Macron wa Ufaransa aitembelea China

3 Desemba 2025

Ufaransa inatarajia kuingia kwenye mikataba kadhaa ya kibiashara na China kupitia ziara ya rais Emmanuel Macron Beijing

https://p.dw.com/p/54hNd
Rais Emmanuel Macron katika ziara mjini Beijing anakotarajia kuzungumza na viongozi kuhusu masuala kadhaa ya ushirikiano
Rais Emmanuel Macron katika ziara mjini Beijing anakotarajia kuzungumza na viongozi kuhusu masuala kadhaa ya ushirikianoPicha: Ludovic Marin/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara ya siku tatu nchini  China ambako amewasili hivi leo, akilenga kujadili na viongozi wa nchi hiyo kuhusu biashara na diplomasia.

Kiongozi huyo wa Ufaransa anataka kuishawishi Beijing kuishinikiza Urusi kuelekea suala la kufikia makubaliano ya usitishaji vita na Ukraine.

Macron kuelekea China kwa mazungumzo na Xi kuhusu uhusiano wa kibiashara na vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Maafisa wa Ufaransa na China wanatarajiwa kwenye ziara hiyo kusaini makubaliano kadhaa katika sekta za nishati, chakula na usafiri wa anga.

Ofisi ya rais Macron imesema, kiongozi huyo atatetea juhudi za kuwepo soko huru lenye kuzingatia haki ya kibiashara.