1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron kuelekea China kwa ziara ya kikazi ya siku tatu

3 Desemba 2025

Rais Emmanuel Macron anaelekea China kwa ziara ya siku tatu inayolenga biashara na mazungumzo ya kidiplomasia, huku rais wa Ufaransa akitaka kuishirikisha Beijing katika kushinikiza Urusi kusitisha mapigano na Ukraine.

https://p.dw.com/p/54ezq
Ufaransa China | Ziara ya Xi Jinping na Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) na Rais wa China Xi Jinping wakipiga picha kabla ya mkutano wa pande mbili wakati wa ziara ya kitaifa ya kiongozi wa China, katika Ikulu ya Élysée mjini Paris, Jumatatu, Mei 6, 2024.Picha: Ludovic Marin/AP/picture alliance

Kwa mjibu wa ofisi yake, Macron atapigania ajenda ya ushirikiano katika masuala ya uchumi na biashara inayolenga kufikia uwiano unaohakikisha "ukuaji endelevu, imara na wenye manufaa kwa wote.” Ufaransa inalenga kuvutia uwekezaji zaidi kutoka kwa kampuni za China na kurahisisha upatikanaji wa masoko kwa bidhaa za Ufaransa. Wakati wa ziara hiyo, maafisa kutoka mataifa yote mawili wanatarajiwa kusaini makubaliano kadhaa katika sekta za nishati, chakula na anga. Ufaransa itakuwa mwenyeji wa mkutano nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 mwaka 2026 unaohusisha uchumi mkubwa zaidi duniani, huku China ikitarajiwa kuongoza jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki (APEC) lenye wanachama 21, wakiwemo Marekani, Korea Kusini, Japan, Australia na Urusi.