1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Raia watano wa Msumbiji wauawa Afrika Kusini

3 Juni 2026

Polisi ya Afrika Kusini inasema raia wawili wa Msumbiji wameuawa kwenye ghasia za mwishoni mwa wiki, huku serikali ya Msumbiji ikisema raia wake watano wameuawa kwenye mashambulizi yanayotokana na chuki dhidi ya wageni.

https://p.dw.com/p/5El2G
Afrika Kusini Johannesburg 2015 | chuki dhidi ya wageni
Moshi ukifuka baada ya maduka ya wageni kuchomwa moto mjini Johannesburg katika kampeni ya chuki dhidi ya wageni.Picha: Kim Ludbrook/dpa/picture alliance

Maandamano dhidi ya wageni wasiokuwa na vibali yamekuwa yakiongezeka katika wiki za hivi karibuni.

Ghana imewahamisha raia wake 300, na Nigeria imetangaza kuchukuwa hatua kama hiyo.

Ghasia zilizuka kwenye mji wa pwani wa Mossel Bay siku ya Ijumaa, ambapo waandamanaji walichoma moto maduka ya raia wa kigeni, wengi wao kutokea mataifa ya Afrika.

Katika taarifa yake ya siku ya Jumatatu, serikali ya Msumbiji ilisema raia wake saba wamefariki dunia nchini Afrika Kusini, watano kati yao wakiwa wameshambuliwa na waandamanaji. Jeshi la polisi limethibitisha vifo viwili tu kati ya hivyo.

Haya ni mauaji ya kwanza kwenye wimbi la sasa la ghasia zinazochochewa na chuki dhidi wa wageni.