1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin: Urusi na China haziundi muungano wa kijeshi

26 Machi 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema leo kuwa nchi yake haiundi muungano wowote wa kijeshi na China na kwamba nchi hizo mbili hazifichi chochote kuhusiana na ushirikiano wao wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4PGcy
Russlands Putin führt Gespräche mit Chinas Xi in Moskau
Picha: SERGEI KARPUKHIN/AFP

Putin amesema pia kuwa Mataifa ya Magharibi yanajaribu kuunda miungano ya kimataifa, huku akiishutumu Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO kwa kuanza kuunda muungano mpya unaofanana na ulioijumuisha Ujerumani, Italia, na Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Soma pia: Xi, Putin wasifu enzi mpya ya mahusiano kati ya mataifa hayo mawili

Mapema wiki hii, Putin na rais wa China Xi Jinping walifanya mkutano wa kilele na kusifu kile walichokitaja kuwa "enzi mpya ya uhusiano" na kuahidi kuimarisha ushirikiano wao. Hayo yanajiri mnamo wakati Urusi inajitahidi kupiga hatua katika uvamizi wake nchini Ukraine.