1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Xi, Putin wasifu enzi mpya ya mahusiano kati yao

Bruce Amani
22 Machi 2023

Viongozi wa China na Urusi wamesifu kile walichokiita "enzi mpya" katika mahusiano yao, wakati wakiuonyesha umoja wao mjini Moscow.

https://p.dw.com/p/4P33M
Russlands Putin führt Gespräche mit Chinas Xi in Moskau
Picha: Sputnik/Mikhail Tereshchenko/Pool via REUTERS

Rais wa Urusi Vladmir Putin alizituhumu nchi za Magharibi kwa kukataa mapendekezo ya Beijing ya kumaliza vita vya Ukraine.

Mataifa hayo, ambayo yana hamu ya kukandamiza nguvu za Magharibi, yalielezea wasiwasi kuhusu utanuzi wa Jumuiya ya NATO barani Asia na kukubaliana kuimarisha ushirikiano ambao umeendelea kuwa wa karibu hata zaidi tangu Putin alianzisha uvamizi nchini Ukraine.

Akizungumza baada ya kukutana na Rais wa China Xi Jinping, Putin alisema yuko tayari kwa mazungumzo kuhusu Ukraine na kuusifu mpango wa China wa ajenda 12 kuhusu mzozo huo, unaojumuisha wito wa mazungumzo na kuheshimiwa uhuru wa mipaka ya nchi zote.

Marekani inasema haiioni China kuwa na uwezo wa kuwa mpatanishi asiyeegemea upande wowote.