1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin: Urusi haitarudishwa nyuma

18 Machi 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake haitatetemeshwa. Ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa baada ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4dqDt
Urusi | Hotuba ya rais baada ya uchaguzi
Putin amesema matokeo ya uchaguzi ni ishara ya imani na matumaini raia wa Urusi wako nayo kwake.Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

Rais huyo wa Urusi amepata asilimia 87,33 ya kura, kulingana na taarifa rasmi iliyotolewa Jumatatu huku asilimia 99 ya kura zikiwa zimehesabiwa.

Katika hotuba yake rais Vladimir Putin amesema matokeo hayo ni ishara ya imani na matumaini waliyokuwanayo raia wa Urusi kwake.

Hata hivyo wapinzani wamesema matokeo hayo ni ishara nyingine ya uchaguzi uliopangwa mapema.

Mshirika mkuu wa Urusi, China imempongeza Putin kwa ushindi wake. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China ameeleza kuwa China na Urusi ni majirani wakubwa na washirika muhimu katika enzi mpya. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amemtaja Putin kuwa ni dikteta mwenye uchu wa madaraka.

Na ikulu ya Marekani imesema uchaguzi wa Urusi haukuwa huru na wa haki.