1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin ajiandaa kwa ziara ya siku mbili nchini China

15 Mei 2024

Rais wa Urusi Vladmir Putin atasafiri kwenda China Alhamisi kwa ziara ya siku mbili itakayotuama juu masuala ya usalama wa ulimwengu na wa kikanda wakati wa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Xi Jinping mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4ftZf
Rais wa Urusi Vladmir Putin mkoani Severodvinsk
Rais wa Urusi Vladmir Putin mkoani Severodvinsk akiwa na kamanda wa vikosi vya wanamaji Nikolai YevmenovPicha: Mikhail Klimentyev/Russian Presidential Press/TASS/dpa/picture alliance

Rais wa Urusi Vladmir Putin atasafiri kwenda China kesho Alhamisi kwa ziara ya siku mbili itakayotuama juu masuala ya usalama wa ulimwengu na wa kikanda wakati wa mazungumzo na mwenyeji wake Rais Xi Jinping mjini Beijing.

Ziara ya kiongozi huyo nchini China inafanyika katika wakati vikosi vyake vimezidisha mashambulizi na vinaendelea kusonga mbele kwenye mkoa wa Kharkiv uliopo mashariki mwa Ukraine.

Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua, leo Jumatano, Putin amesema utawala wake uko tayari kufanya mazungumzo kuhusu mzozo wa Ukrainechini ya masharti ya kuyajumuisha matakwa ya Urusi. Hata hivyo pendekezo hilo la Putin limekataliwa mara moja na utawala wa Ukraine.

Akiwa nchini China, Putin na Xi watajikita katika kujadili njia za kutanua zaidi ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuupiku upande wa magharibi unaongozwa na Marekani.