1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Putin aunga mkono mpango wa China wa kuutatua mzozo Ukraine

15 Mei 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin, katika mahojiano yaliyochapishwa leo, amesema anaunga mkono mpango wa China wa kuutatua kwa njia ya amani mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4frH6
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Sputnik/Pavel Byrkin/Kremlin/REUTERS

Katika mahojiano hayo, Putin ameeleza kuwa China ina ufahamu kamili wa kilichosababisha mzozo huo na maana yake katika siasa za kijiogrofia.

Akizungumza na shirika la habari la serikali ya China Xinhua kuelekea ziara yake mjini Beijing wiki hii, Putin amesema Urusi bado imeacha milango ya mazungumzo wazi ili kuutatua mzozo huo uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Soma pia: Vladmir Putin: Urusi haitaruhusu vitisho 

China ilitoa mapendekezo yenye nukta 12 ya kuumaliza mzozo huo zaidi ya mwaka mmoja uliopita lakini haikufafanua zaidi kwa undani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov mwezi uliopita alilitaja pendekezo la kuutatua mzozo wa Ukraine kama "mpango wa busara wa ustaarabu wa China kwa ajili ya kujadiliwa."