Olimpik ya walemavu kuanza Beijing | Michezo | DW | 28.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Olimpik ya walemavu kuanza Beijing

Wanariadha 400 walemavu watawasili beijing kwa michezo yao ya olimpik Septemba 6-17.

Punde tu kumalizika kwa michezo ya 29 ya Olimpik ya Beijing,juzi jumapili, China, wenyeji, wameanzisha jana mbio za mwenge wa olimpik za siku 10 kwa michezo ya walemavu ya olimpik-"Paralympic Games"itakayfanyika Beijing kuanzia Septemba 6 hadi 17 ikihudhuriwa na wanariadha-walemavu kiasi cha 4,000 .

Kabumbu likirudi sasa usoni uwanjani na Ligi za Itali na Spain zikianza msimu mpya mwishoni mwa wiki hii,mabingwa wa Ujerumani-Bayern Munich ambao wameanza vibaya katika Bundesliga,wanapanga kumuajiri beki mshahara wa Itali Massimo Oddo kutoka klabu bingwa AC Milan. Mahasimu wao Hamburg ,wanatazamiwa kutangaza mnamo siku 2 hizi kumuajiri mbrazil Thiago Neves ili kuimarisha kikosi chao kwa Bundesliga:

►◄

Michezo ya olimpik ya kawaida ikiwa imefungwa rasmi jumapili iliopita na kuitwa wanariadha wakike na kiume kujikusanya tena miaka 4 kutoka sasa mjini London,kwa michezo ya 2012, China imegeukia sasa michezo ya olimpik kwa walemavu.Mwenye wa kuanzisha michezo hiyo ulianza jana mbio zake za siku 10 ukichukuliwa na jumla ya wabebaji 850 kupitia nji 2 -moja ya kale na nyengine ya kisasa katika miji 11 ya China kabla ufunguzi rasmi wa michezo hii ya 13 ya walemavu hapo Septemba 6.

Kiasi cha wanariadha 4.000 wanatazamiwa kutamba Beijing na waandazi wa michezo hii wanasema tiketi zimeshauzwa kwa Uwanja mkuu wa kyota cha ndege mjini Beijing.Hatahivyo, kiasi cha nusu cha tiketi hazijauzwa bado.

Tiketi za uwanja mkuu wa Kyota zimeuzwa zote isipokuwa nusu ya tiiketi katika viwanja vyengine hazikutoka.Kiasi cha mashabiki 350,000 watasaidia kuwashangiria walemavu wakinyanganyia nao medali za dhahabu,fedha na shaba.

Baada ya kumalizika pia Olimpik mwishoni mwa wiki iliopita,macho ya mashabiki yanakodolewa tena mwishoni mwa wiki hii viwanja mbali mbali vya dimba.Wakati Bundesliga-Ligi ya Ujerumani imeshaanza tangu wiki 2 zilizopita,Ligi za Itali na Spian zarudi uwanjani kwa msimu mpya mwishoni.

Bayern Munich, mabingwa wa Ujerumani, walianza kwa sare mara mbili za bao 1:1.Ni klabu ya daraja ya pili iliopanda ya kwanza, Hoffenheim, ndio inayoongoza orodha ya Ligi.Kubadili mkosi huu, Munich imepanga kumuajiri mlinzi wa Itali Massimo Oddo kutoka klabu bingwa -AC Milan.Hii ni kwa muujibu vile Munich ilivyoarifu jana.

Mlinzi huyo wa kulia Oddo anaazimwa tu lakini kwa kipindi cha mwaka mmoja.Akiwa na umri wa miaka 32, Oddo anajiunga na mtaliana mwenzake mshambulizi hatari kutoka pia Itali-Luca Toni.

Mpatano haya yamekuja siku moja baada ya Bayern Munich kumuuza mlinzi wake wa shoto kwa Hamburg kwa kitita cha Euro milioni 8.Oddo ameichezea timu ya taifa ya Itali mara 31 na alikuwamo ndani ya timu iliotawazwa mabingwa wa dunia 2006 Ujerumani.

Nayo Ligi ya Itali-serie A inaanza mwishoni mwa wiki hii kwa changamoto 2 za kusisimua:Juventus ina miadi na Fiorentina timu zilizomaliza nafasi ya 3 na ya 4 msimu uliopita hapo jumapili huko Florence.huu utafuatia mpambano wa kukata na shoka wa jumamosi mjini Roma kati ya Roma na Napoli.

Inter Milan inapigana kupata mlinzi wakati imara kwa mpambano wake wa jumamosi na Sampdoria.

La Liga-ligi ya Spian,mabingwa wa Ulaya mwaka huu, inaanza kwa zahama kali kwa Real Madrid kuchuana na Deportivo La Coruna hapo jumapili.

Real wanaiogopa sana deportivo zaidi kuliko FC barcelona au hata Valencia,kwani Real haikutamba mbele ya deportivo la coruna tangu 1991.Pia imeshindwa ilipozuru huko mara 5 zilizopita.