Ofisi ya Hillary Clinton yatekwa kwa muda na mtu anayehisiwa punguani | Habari za Ulimwengu | DW | 01.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ofisi ya Hillary Clinton yatekwa kwa muda na mtu anayehisiwa punguani

NEW HAMPSHIRE.Mwanaume mmoja akiwa na kitu alichodai ni bomu ameingia katika ofisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Democrat nchini Marekani, Hillary Clinton na kuwashikilia mateka wafanyakazi wa ofisi hiyo.

Hata hivyo mzozo huo umemalizika bila ya madhara yoyote baada ya mtu huyo kujisalimisha kwa polisi. Hillary Clinton hakuwepo ofisini wakati wa tukio hilo.

Mtu huyo akiwa na kitu alichodai ni bomu aliingia katika ofisi hizo zilizoko Rochester New Hampshire akitaka kuonana na mgombea huyo Hillary Clinton ambapo aliwashikilia mateka wafanyakazi wa ofisi hiyo kwa muda wa saa sita.

Yaarifiwa kuwa mtu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 ana historia ya maradha ya akili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com