Obama atuma kikosi cha washauri wa kijeshi Uganga | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.10.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Obama atuma kikosi cha washauri wa kijeshi Uganga

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa anapeleka kikosi cha washauri wa kijeshi 100 nchini Uganda kusaidia majeshi ya eneo hilo yanayomsaka kiongozi wa LRA Joseph Kony.

default

Rais wa marekani Barack Obama ametuma kikosi cha wanajeshi nchini Uganda.

Katika barua kwa baraza la Congress jana Ijumaa, rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa anapeleka kiasi washauri wa kijeshi 100 nchini Uganda kusaidia majeshi ya eneo hilo ambayo yanamtafuta Joseph Kony pamoja na makamanda wengine wa kundi la Lord's Resistance Army, LRA. Obama amesema kuwa ameidhinisha idadi ndogo ya wanajeshi kusaidia kumuondoa kiongozi huyo wa Lord's Resistance Army kutoka eneo la mapambano. Hata hivyo amesema, licha ya kuwa kikosi hicho kitakuwa na silaha lakini wanajeshi hao watatoa tu taarifa, ushauri na msaada kwa majeshi ya mataifa washirika.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com