Nusu-finali ya champions League | Michezo | DW | 21.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Nusu-finali ya champions League

Wakati kocha wa afrika kusini Parreira ajiuzulu,mashabiki wa ulaya wakodoa macho leo kwa nusu-finali ya champions league.

Wakati ulimwengu wa dimba barani Afrika umegubikwa na taarifa za kujiuzulu kwa kocha wa Afrika kusini kutoka Brazil,Carlos Alberto Parreira,mashabiki wa dimba wa Ulaya wanajiandaa kwa nusu-finali ya leo na kesho ya champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Nusu finali ya kwanza leo inazikumbanisha timu 2 za Uingereza:FC Liverpool ikicheza nyumbani dhidi ya Chelsea.

Kesho itakua zamu kati ya FC Barcelona ya Spian na Manchester United.

Kocha wa Bafana bafana -Afrika kusini mbrazil Carlos Parreira alietazamiwa kuiongoza hadi kombe lijalo la dunia, ameamua kuiacha mkono Afrika kusini.Gazeti la jumapili la Sunday Times liliripoti kuwa mke wa Parreira -Leila, anaugua maradhi ya kensana hivyo mumewe ataka kumshughulikia.

Carlos Alberto Parreira aliongoza Brazil kutwaa kombe la dunia 1994 nchini Marekani.Afrika kusini ikiandaa kombe hilo nyumbani ilimchagua yeye aiandae kwa kombe hilo.

Amepitisha miezi 16 tu kama kocha wa Bafana Bafana .

Nani atajaza pengo lake,ni swali la kusubiri na kuona.

Nusu-finali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kati ya leo na kesho ni kati ya klabu 3 za Uingereza na 1 ya Spian.Leo wanaanza kinyan'ganyiro cha kuania nafasi ya finali wenyewe kwa wenyewe waingereza:FC Liverpool yaumana na Chelsea wakati kesho mabingwa wao Manchester United wana miadi na FCBarcelona ya Spian.

Swali ni je, waingereza watapata pigo la msimu uliopita pale timu 1 ya Itali-Ac Milan ilipozitoa timu pia za uingereza na kutoroka na kombe au Manchester,Chelsea au hata Liverpool zitatoroka na kombe hili tena hadi visiwani .

Jambo moja lafahamika wazi sasa-watatu kati ya makocha 4 wa timu hizi 4 zinazocheza nusu-finali karibu yamkini wakatimuliwa tena hata wakitwa kombe hilo mwezi ujao.

Ni Sir Alex Ferguson tu wa Manchester mwenye uhakika wa kubakia na hatamu wakati wenzake Frank Rijkaard wa Barcelona, Avram Grant wa Chelsea na Rafa Benitez wa Liverpool,waweza wakapigwa kumbo.

Miaka ya nyuma kuiongoza timu hadi hatua ya nusu-finali ikionekana ni ufanisi mkubwa, leo lakini ni kutawazwa tu mabingwa ndiko kunakohesabiwa.Mashabiki wa FC barcelona wana kiu cha kombe jengine la ulaya kufuatia ushindi wao wa 2006 walipoilaza Arsenal na kutwa kombe mjini Paris.

Kocha Rijkaard ameiangalia Fc Barcelona ikipepesuka nyumbani katika mapambano yakle 2 yaliopita:Ilitoka sare 0:0 na Getafe na tena na Barcelona Espanyol.Katika mechi 8 zilizopita za la Liga, Barcelona ilimudu ushindi mmoja tu na hii ikaifungulia mlango Real Madrid kuparamia kileleni bila taabu.

Vyombo vya habari vya Spain vimevumisha kwamba mpambano wa kesho na MANU huenda ukawa wa mwisho kwa Rijkaard ikiwa Barcelona itashindwa kutamba mbele ya Manchester.

Mwenzake Benirez wa Liverpool,alieiongoza kutwaa kombe hili la ulaya 2005 bila ya kutazamiwa na kuiongoza tena finali ya kombe hili mwaka jana ilipolazwa na AC Milan ya Itali, huenda akachukua yeye usukani wa Barcelona.Licha ya kupendwa na mashabiki wa Liverpool licha ya kutowatawaza mabingwa nyumbani tangu 1990,Benitez huenda akafikiri wakati umewadia wa kufunga virago na kuelekea kwengine.

Hali upande wa Chelsea ni tofauti,kwani huko bilionea wa kirusi ana mamlaka kamili ya kuamua na hadi sasa amenyamaa kimya juu ya hatima ya rafiki yake Avram Grant aliechukua usukani kwa Jose Mourinho.Grant ameshindwa mara 5 tu katika mapambano 48 tangu kuchukua uongozi kutoka kwa Mourinho.

Ushindi leo dhidi ya Liverpool utaichukua Chelsea na akina Essien na drogba kwa mara ya kwanza katika finali ya kombe hili la klabu bingwa barani Ulaya.Na hayo yatakua mafanikio yao ma,kubwa tangu Chelsea kuasisiwa miaka 103 iliopita.