Nini hatma ya Opel ? | Magazetini | DW | 25.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Nini hatma ya Opel ?

Uamuzii upo kwa General Motors au kwa Kanzela ?

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumanii hii leo yamegusia mada mbali mbali ,nyngi za ndani nchni:Hatima ya kwanda cha magari cha Opel na uamuz unaosubriwa kwa hamu kutoka General Motors;mkasa wa Kanzela Angela Merkel kumuandalia party ya siku ya kuzaliwa mkuu wa Deutsche Bank na marafiki zake Ikulu na chaguzi za mikoa 3 ya Ujerumani mwishoni mwa wiki hii ambazo zitatoa ishara ya mkondo wa uchaguz mkuu ujao:Munchner Merkur laandika:

"Alao hadi ule usiiku wa kucheza kamar katika afs ya Kanzela,Bibi merkel na makamo wake Bw.Steinmeier walpaswa kungamua wamarekani wanatumia kila silaha walionayo kujvutia upande wao.Iilikuwa dhahrii-shahrii tangu mwanzo kuwa Kampuni (mama) la General motors halikua na azma kuliachia taw lake la Opel na kuona haki-milk zinaelekea Russa. General Motors linahyari kwahivyo, kuendeleza ushiriikiano na mwekezaji RHJ,mpinzani wa kampuni la Magna."

Likiendeleza mada hii, gazeti la LEIPZGER VOLKSZETUNG- linaandika kuwa, ni General motors pekee inayoweza kuamua wapo iuze au la, tawi lake la i Opel.Laandka:

Uwezo wa Kanzela (Merkel) hapo ni mdogo katika mazungumzo ya uso kwa uso na Rais Obama kufankiiwa yale atakayo.Na ikiwa mtetezi wa wadhfa wa ukanzela wa chama cha SPD -Bw.Steinmeier amezungumza na wazri mwenzake wa mambo ya nje wa Marekanii Bibi Hillary Clinton au la, hakuna umuhmu wowote .IIkiwa lakini GM itaamua kushirikiana na kampuni la Kanada (Magna) , n kwa kuwa tu seriikalii ya Ujerumani italipa bei kubwa zadi kwa njia ya kutoa dhamana ya kiseriikali,mkopo au fdia.Muda mfupi kabla ya uchaguzii wa Ujerumani, ni kpindi kizuri kucheza kamari.

Likitugeuziia mada, gazeti la SAARBRUCKER ZEITUNG linazungumzia mkasa wa mkuu wa Deutsche Bank ,Ackerman kufanyiwa party Ikulu .Gazet laandiika:

Vichwa vya habarii vilvyohanikza juu ya patry ya kusherehekea siku ya kuzaliwa mkuu wa Deutsche Bank,Bw.Ackermann,havitampendeza Kanzela Angela Merkel.Bila shaka, ni ruhusa kwa Kiongozi wa serikali ,lasema gazetii- kuwaalika wageni Ikulu ili kuwa na mahusiano mema.Swali linazuka pale milionea huyo pamoja na marafiki walochaguliwa maalumu kualikwa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa gharama za walipaji kodi.

Wazirii wa afya Bibi Ulla Schmidt, tayari kwa kutumia motokaa ya wizara yake kwa likizo,amewachemsha watu kwa hasira.Iililobaki ni kuona iwapo watu na vyombo vya habarii sasa vitamlenga Kanzela Merkel kwa mwaliko wake wa ukarimu.

Likituhetimishiia uchambuzii huu wa maoni ya wahariri, gazeti la NEUE OSNABRUCKER ZEITUNG linazungumzia uchaguzi katika mikoa 3 mwishon mwa wiki hii:Laandika:

Nguvu zote walizotuma watetezi wake katika kampeni ya uchaguzi,hazikuksaida chama cha SPD hadi sasa kujikomboa.Msaada sasa unatazamiiwa kutoka mikoa ya Saarland na Thüringen.Kuangushwa kwa waziri mkuu wa chama cha CDU kabla ya uchaguzi mkuu ujao , kungekuwa mafanikio ya kutiia moyo ambayo mtetezi wa SPD kwa ukanzela Bw.Stenmeier angehitajii mno.

Kufikia shabaha hiyo, yuko hata tayari kuungana na vyama vya mrengo wa shoto zaiidi (Linkspartei) hata mkoani Saarland na hata ikiwa huko Bw.Lafontaiine atakuwa ndie mshrika wao.hicho nii kroja cha mambo cha histora. (Bw.Lafontein alkacha-mkono chama cha SPD).

Mwandishi:Ramadhan Ali/Dt Zeitungen

Mhariri:M.Abdul-Rahman