1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Korea ya Kaskazini kuwekewa vikwazo?

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4J

Wajumbe wa nchi tano ,wanachama wa kudumu kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekutana kutafakari vikwazo dhidi ya Korea ya Kaskazini kufuatia hatua ya nchi hiyo kufanya jaribio la silaha za nyuklia.

Wajumbe hao wa Marekani,Urusi, Ufaransa, Uingereza na China wanajadili mswada wa azimio uliowasilishwa na Marekani muda mfupi tu baada ya Korea ya Kaskazini kufanya jaribio hilo.

Hapo awali baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililaani vikali jaribio hilo.