NEW YORK: Wito kwa Cyprus kuanzisha majadiliano ya kuungana | Habari za Ulimwengu | DW | 07.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Wito kwa Cyprus kuanzisha majadiliano ya kuungana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon ametoa wito kwa Cyprus iliyogawika kati ya watu wenye asili ya Kigiriki na Kituruki,kufanya majadiliano ya dhati kukiunganisha tena kisiwa hicho cha Bahari ya Mediterania. Amesema, inasikitisha kuwa mwaka mmoja baada ya kukubali kuanzisha majadiliano moja kwa moja,hakuna kilichofanywa.Katibu Mkuu Ban akaongezea kuwa suluhisho linapaswa kutoka kwa Wacyprus wenyewe, lakini Umoja wa Mataifa upo tayari kusaidia juhudi za kutafuta suluhisho.Majadiliano ya upatanisho kati ya pande mbili za Cyprus yamekwama tangu mwaka 2004.Wakati huo sehemu ya wakaazi wenye asili ya Kigiriki ilipinga suluhisho lililopendekezwa na Umoja wa Mataifa.Tarehe 8 Julai mwaka 2006,pande zote mbili zilikubali kufufua majadiliano yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com