1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Wapakistani wakabiliwa na kitisho cha baridi kali baada ya nyumba zao kubomolewa na tetemeko.

14 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESB

Umoja wa mataifa umeeleza wasi wasi wake kutokana na hali inayoendelea kuwa mbaya inayowakabili mamia kwa maelfu ya Wapakistani ambao wanalazimika kuishi katika maeneo ya wazi tangu pale lilipotokea tetemeko la ardhi na kuharibu nyumba zao.

Mratibu mkuu wa masuala ya misaada ya dharura wa umoja wa mataifa Jan Egeland ameielezea hali hiyo kuwa ni ya kuogofya wakati majira ya baridi kali ikikaribia.

Egeland amesema pia kuwa helikopta zaidi zinahitajika kuweza kuwafikia watu wanaoishi katika maeneo ya milima ya Himalaya.