NEW YORK : Hukumu ya kifo yampa wasi wasi Annan | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Hukumu ya kifo yampa wasi wasi Annan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameelezea wasi wasi wake kwa uamuzi wa mahkama ya Libya kuwahukumu tena adhabu ya kifo wafanyakazi sita wa matibabu waliopatikana na hatia ya kuwaambukiza watoto wa Libya virusi vya HIV.

Katika taarifa yake Annan amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia mahitaji ya watoto hao walioathirika na kutafuta suluhisho la ubinaadamu kwa hatima ya wafanyakazi hao wa matibabu.

Taarifa hiyo ya Annan inafuatia shutuma za kulaani hukumu hiyo kutoka kwa Rais George W. Bush wa Marekani na viongozi wa Ulaya ambao wamekasirishwa na hukumu hiyo ya kifo dhidi ya wauguzi sita wa Bulgaria na daktari mmoja wa Kipalestina.

Inadaiwa kwamba hukumu hiyo ya kifo imetolewa licha ya kuwepo kwa ushahidi wa kisayansi kwamba watoto hao waliambukizwa virusi hivyo kabla wafanyakazi hao wa matibabu kuwasili nchini Libya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com