NEW DELHI: India yajaribu kombora linaloweza kubeba mabomu ya kinuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI: India yajaribu kombora linaloweza kubeba mabomu ya kinuklia

India imefanikiwa kujaribu kombora la masafa ya wastani ambalo huweza kupachikwa mabomu ya kinuklia.Kwa mujibu wa afisa katika wizara ya ulinzi,kombora la Prithvi II lilirushwa kutoka jimbo la pwani ya mashariki la Orissa.Jaribio hilo limefanywa siku tatu baada ya Pakistan kufanya jaribio la kombora lake la Ghauri linaloweza kubeba mabomu ya kinuklia.India iliarifiwa na Pakistan kuhusu jaribio hilo na wakati huo Pakistan ikasema kuwa inaitazamia India kufanya jaribio lake hivi karibuni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com