1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege za kivita za serikali ya Syria zahujumu Idlib

Oumilkheir Hamidou
2 Desemba 2019

Hujuma za angani dhidi ya soko moja katika mkoa wa kaskazini magharibi mwa Syria unaodhibitiwa na waasi, Idlib, zimeangamiza maisha ya watu wasiopungua 10 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/3U6AX
Syrien Konflikt l Zahlreiche Tote nach Kämpfen in Idlib
Picha: Getty Images/O. H. Kadour

Hujuma hizo zimetokea katika wakati ambapo visa vya Soldat in Syrienmatumizi ya nguvu vimezidi huko Idlib-ngome ya mwisho ya upinzani ambako mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yamepelekea dazeni kadhaa za watu kuuliwa kutoka pande zote mbili mwishoni mwa wiki.

Shirika linalosimamia masuala ya haki za binaadam nchini Syria, lenye makao yake nchini Uingereza, limesema ndege za kiivita zimelihujumu soko moja katika mji wa Maaret al-Numan na kuwauwa watu 10, Kituo cha  kukusanya habari cha Aleppo-shirika la wanaharakati , kimeripoti pia kuhusu idadi hiyo hiyo ya wahanga  huku shirika la hifadhi ya jamii ambalo ni sehemu ya upande wa upinzani, linalojulikana kama "Vikofia vyeupe"linazungumzia kuhusu raia tisa waliouliwa, wakiwemo wanawake wawili.

Mashambulio karibu na mpaka wa Uturuki
Mashambulio karibu na mpaka wa UturukiPicha: Getty Images/AFP/N. al-Khatib

Ripoti zinatofauatiana kuhusu idadi ya wahanga

Shirika hilo linasema watu 13 wakiwemo watoto wawili, wamejeruhiwa. Limeongeza kusema idadi halisi ya waliouliwa bado haijulikani. Katika mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni jambo la kawaida  kwa watu kuzungumzia kuhusu idadi tofauti ya watu waliouliwa .

Hujuma za mabomu katika soko hilo zililengwa kuangamiza maisha ya watu wengi na kusababisha uharibifu mkubwa zaidi-shirika hilo la hifadhi ya jamii limesema kupitia ukurasa wake wa Facebook zikiwemo picha za wahanga tangu waliouliwa mpaka wale waliojeruhiwa ambao wanahudumiwa na wauguzi.

Shirika linalosimamia masuala ya haki za binaadam na jengine la hifadhi ya jamii yamezungumzia kila moja kwa upande wake kuhusu hujuma hizo za ndege katika mji wa karibu na hapo wa Saraqeb wakisema watu kadhaa wameuliwa na wengine kujeruhiwa.

Vikosi vya serikali ya Syria vinafanya hujuma za angani tangu miezi minne iliyopita huko Idlib, mkoa unaodhibitiwa na wanamgambo wanaoelemea upande wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida. Hujuma hizo za vikosi vya serikali zimewalazimisha malaki ya watu kuyahama maskani yao.

Makubaliano tete ya kuweka chini silaha yalivizuwia vikosi vya serikali kusonga mbele mwezi Agosti uliopita, lakini mnamo wiki za hivi karibuni makubaliano hayo mara kwa mara yamekuwa yakivunjwa.

Wanajeshi wa Urusi mjini Damascus
Wanajeshi wa Urusi mjini DamascusPicha: Reuters/O. Sanadiki

Shambulio dhidi ya wanajeshi wa Urusi na Uturuki karibu na Kobani

Wakati huo huo maafisa watatu wa kijeshi wa Urusi wamejeruhiwa bomu liliporipuka katika mji wa mpakani wa Kobani ambako vikosi vya Urusi na vile vya Uturuki vinashirikiiana kupiga doria tangu mwezi uliopita.

Maafisa hao wa kijeshi walikuwa wanatathmini uwezekano wa kufungua njia nyengine ya kupiga doria wakiwa ndani ya gari la kijeshi pale bomu liliporipuka-wizara ya ulinzi imesema.