1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaionya Urusi kuwa itatumia njia zote kujilinda

23 Septemba 2025

Jumuiya ya Kujihami NATO imeionya Urusi hii leo kwamba, itatumia njia zote kujilinda dhidi ya ukiukaji wowote zaidi wa anga yake baada ya matukio mawili ya urushwaji wa ndege za droni za Urusi.

https://p.dw.com/p/50yEF
Brüssel 2025 | NATO-Katibu Mkuu Mark Rutte
Katibu Mkuu wa NATO Mark RuttePicha: Geert Vanden Wijngaert/REUTERS

Jumuiya ya Kujihami NATO imeionya Urusi hii leo kwamba, itatumia njia zote kujilinda dhidi ya ukiukaji wowote zaidi wa anga yake baada ya matukio mawili ya urushwaji wa ndege za droni za Urusi. Tukio la kwanza ni la kudunguliwa mapema mwezi huu kwa ndege za Droni za Moscow katika anga ya Poland na ripoti za wiki iliyopita za anga ya Estonia kuingiliwa na ndege za kivita za Urusi. Estonia ilisema ndege tatu za kivita za Urusi ziliingia anga lake kwa dakika 12 tu siku ya Ijumaa bila kuruhusiwa, madai ambayo Urusi imeyakanusha. Matukio yote hayo yamewashutua viongozi kote barani Ulaya na kuibua maswali juu ya jinsi gani mataifa hayo yamejiandaa kujilinda dhidi ya uchokozi wa Urusi unaozidi kuongezeka.